Jumanne, 17 Juni 2014

Tusisubiri kesho kufanya yale tunayopaswa kufanya.Tufanye SASA, LEO si Baadae wala KESHO

Yapo mambo mengi sana tunayopaswa kujifunza kwayo. Mojawapo ni pale mmoja kati ya watu tuliokuwa tumezoeana nao,tulioishi nao,tuliofurahi nao,hata wale tuliokuwa maadui wanapotutoka na kwenda mahala ambapo hatuwezi kuwa na mawasiliano nao tena katika mwili huu wa nyama. Hebu jiulize ni maneno yapi yatasemwa na watu kuhusu wewe wakiimaanisha utakapokuwa umeondoka ? tafakari kidogo. Je, watakukumbuka kwa mengi mazuri au watakupa sifa bubu zisizo na uhai katika dunia hii ?. 

Ndugu zangu Mungu ametupa akili tuzitumie ipasavyo SASA,LEO na si baadae au kesho.Tufanye hivyo kwa mazuri tena bila kuchelea maana hatujui siku wala saa. 

Ndugu, rafiki, tungeanza wote mtihani wa kuhitimu Chuo kikuu june/2014, Lakini haiko hivyo tena. Utakumbukwa daima.Amen

Wana CCT RUCO  na familia ya wana RUCO pamoja na familia ya marehemu, wakiomboleza msiba wa mwanajumuia mwenzao Ndugu SUBILI KILASI aliyekuwa mwanachuo kitivo cha sanaa na sayansi ya jamii aliyefariki siku ya ijumaa ya tarehe 8/11/2013. Katika utumishi wa kanisa, marehemu Kilasi alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya chakula na Mwanakwaya wa kwaya ya HOPE akimsaidia m/kit wa nidhamu katika kwaya ya HOPE na aliyemtumikia Mungu kwa nguvu zake zote kwa njia ya uimbaji mpaka mauti yanamkuta. Hakika ni pengo kubwa lakini katika Kristo tunayo imani kuwa Mungu aliifurahia kazi yake aliyoifanya kuwahubiri watu kwa njia ya uimbaji.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Kilasi ukiwa nyumbani kwao
 Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu kuelekea kwenye nyumba yake ya milele
 Safari ya mwisho ya kumpeleka marehemu kilasi kuelekea kwenye nyumba yake ya milele
 Wana CCT pamoja na wanachuo katika safari ya kulekea makaburini
 Mwinjilisti akiongoza safari ya kuelekea makaburini kumsindikiza ndugu Kilasi kwenye makazi yake ya milele



Mama mzazi wa marehemu na Waombolezaji wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la marehemu Kilasi


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni