Jumanne, 17 Juni 2014

UKWATA MKOA WA IRINGA 2014




Hawa ndio viongozi wapya wa UKWATA MKOA WA IRINGA.

Tusisubiri kesho kufanya yale tunayopaswa kufanya.Tufanye SASA, LEO si Baadae wala KESHO

Yapo mambo mengi sana tunayopaswa kujifunza kwayo. Mojawapo ni pale mmoja kati ya watu tuliokuwa tumezoeana nao,tulioishi nao,tuliofurahi nao,hata wale tuliokuwa maadui wanapotutoka na kwenda mahala ambapo hatuwezi kuwa na mawasiliano nao tena katika mwili huu wa nyama. Hebu jiulize ni maneno yapi yatasemwa na watu kuhusu wewe wakiimaanisha utakapokuwa umeondoka ? tafakari kidogo. Je, watakukumbuka kwa mengi mazuri au watakupa sifa bubu zisizo na uhai katika dunia hii ?. 

Ndugu zangu Mungu ametupa akili tuzitumie ipasavyo SASA,LEO na si baadae au kesho.Tufanye hivyo kwa mazuri tena bila kuchelea maana hatujui siku wala saa. 

Ndugu, rafiki, tungeanza wote mtihani wa kuhitimu Chuo kikuu june/2014, Lakini haiko hivyo tena. Utakumbukwa daima.Amen

Wana CCT RUCO  na familia ya wana RUCO pamoja na familia ya marehemu, wakiomboleza msiba wa mwanajumuia mwenzao Ndugu SUBILI KILASI aliyekuwa mwanachuo kitivo cha sanaa na sayansi ya jamii aliyefariki siku ya ijumaa ya tarehe 8/11/2013. Katika utumishi wa kanisa, marehemu Kilasi alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya chakula na Mwanakwaya wa kwaya ya HOPE akimsaidia m/kit wa nidhamu katika kwaya ya HOPE na aliyemtumikia Mungu kwa nguvu zake zote kwa njia ya uimbaji mpaka mauti yanamkuta. Hakika ni pengo kubwa lakini katika Kristo tunayo imani kuwa Mungu aliifurahia kazi yake aliyoifanya kuwahubiri watu kwa njia ya uimbaji.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Kilasi ukiwa nyumbani kwao
 Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu kuelekea kwenye nyumba yake ya milele
 Safari ya mwisho ya kumpeleka marehemu kilasi kuelekea kwenye nyumba yake ya milele
 Wana CCT pamoja na wanachuo katika safari ya kulekea makaburini
 Mwinjilisti akiongoza safari ya kuelekea makaburini kumsindikiza ndugu Kilasi kwenye makazi yake ya milele



Mama mzazi wa marehemu na Waombolezaji wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la marehemu Kilasi


Ijumaa, 4 Aprili 2014

ALBUM YA KWANZA HOPE CHOIR

Hii ni album yao ya kwanza iitwayo MAISHA,ambayo imekuwa ikishika kasi katika mkoa huu wa Iringa.
 Kasha la mkanda wa video wa Hope Choir CCT RUCO
Kasha la mkanda wa Audio wa Hope Choir CCT RUCO

Hope choir wakijifua kwa ajili ya pasaka

Baadhi ya wanakwaya ya Hope (CCT-RUCO) wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya sherehe za pasaka na mikesha ya joint fellowship mkoani Iringa.
Kikundi hiki kimekuwa kikifanya vizuri katika tasnia ya uimbaji katika mkoa huu wa Iringa na hivyo kukiwezesha kupata mialiko mbalimbali yakiwemo matamasha,mikutano,sherehe za harusi,na shughuli zingine.

 Mwalimu wa kwaya Imani S.Nkolela (shati nyeupe) akiwaelekeza na kuwafundisha wanakwaya.kulia kwake ni m/kiti Laurence Mwamakula akiseti mziki kwenye laptop na katikati ni mdau wa Hope choir Jofrey.
Kwa mbali ni Batungulu Yona akifurahi na kushoto kushoto ni Ibrahim Issa